Vacancy title:
17 Msaidizi wa Ofisi TGOS. A
Jobs at:
The United Republic Of Tanzania Registered Judgment ServiceDeadline of this Job:
21 May 2020
Summary
Date Posted: Thursday, May 07, 2020 , Base Salary: Not Disclosed
JOB DETAILS:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
UMOJA NA TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 195
Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011 inaipa Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na majukumu yake mengine, mamlaka ya kuajiri watumishi wa Mahakama wa kada mbalimbali.
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapa chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Mahakama ya Tanzania kwenye Mikoa na Wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi.
Kazi za Msaidizi wa Ofisi
• Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani
• ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo.
• Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofisa wanaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
• Kusambaza barua za ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
• Kutayarisha chai ya ofisi.
• Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
• Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinawekwa sehemu inayostahili.
• Kufungua milango na madirisha ya ofisi wakati wa asubuhi na jioni kuyafunga baada ya saa za kazi.
• Kudurufu barua au machapisho kwenye mashine za kudurufia.
• Kuweka majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.
• Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika
Job Skills: Not Specified
Sifa za Kuingilia Moja kwa Moja
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati
Job Education Requirements: Not Specified
Job Experience Requirements: Not Specified
Work Hours: 8
{module 312}
Job application procedure
Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 21/05/2020 saa 9:30 Alasiri.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi pamoja na namba ya simu na kuambatisha:
- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo. - Wasifu wa mwombaji (CV).
- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
- Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni ambazo zimeandikwa majina nyuma yake .
NB. Nakala za vyeti vya taaluma na vya kidato cha nne/ sita vithibitishwe na Hakimu/Wakili anayetambuliwa na Serikali (True copies of the originals).
Aidha, inasisitizwa kwamba:
• Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44
• Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa Wilaya anayoishi mwombaji.
• Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.
• Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.
• Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania.
• Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE.
• Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.
• Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha watakazotumia maombi yao.
• Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma.
• Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi moja.
• Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao hayatashughulikiwa.
• Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391, DAR ES SALAAM.
Imetolewa na ;
Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391, DAR ES SALAAM,
All Jobs
{module 316}
Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.