Mkufunzi II Job at Public Service Recruitment Secretariat - Career Opportunity in Tanzania

Vacancy title:
Mkufunzi II

[ Type: FULL TIME , Industry: Public Administration, and Government , Category: Civil & Government ]

Jobs at:

Public Service Recruitment Secretariat

Deadline of this Job:
23 February 2021  

Duty Station:
Within Tanzania , Dar es Salaam , East Africa

Summary
Date Posted: Thursday, February 11, 2021 , Base Salary: Not Disclosed


JOB DETAILS:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/L/30 09 Februari, 2021
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Lushoto, Ngara, Nzega, na Mpanda anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi kumi na moja(11) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili. .

MAJUKUMU YA KAZI
• Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo kwa wanafunzi wa astashahada na stashahada;
• Kuendesha mafunzo kwa kozi za uhandisi ujenzi kwa wanafunzi wa astashahada na stashahada;
• Kuandaa michoro na makadrio ya kazi za ujenzi;
• Kusimamia na kukagua kazi za ujenzi zinazofanywa na taasisi;
• Kutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu;
• Kusimamia wanafunzi wakati wa mafunzo kwa vitendo;
• Kufanya tafiti mbalimbali zinazohusiana na kazi za ujenzi;
• Kutekeleza kazi zingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi


Job Skills: Not Specified


SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Uhandisi Ujenzi (Civil Engineering) wenye G.P.A ya 3.5 na kuendelea kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.


Job Education Requirements: Not Specified


Job Education Experience: Not Specified


Work Hours: 8

 

{module 312}

Job application procedure
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
• Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.
• Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
• Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
• Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
• Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
• Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE). • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
• Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
• Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
• Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 23, Februari, 2021.
• Muhimu, kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P. 2320 DODOMA.
• Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/  (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
• Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
LIMETOLEWA NA;
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA


All Jobs

QUICK ALERT SUBSCRIPTION

{module 316}

Job Info
Job Category: Government jobs in Tanzania
Job Type: Full-time
Deadline of this Job: 23 February 2021
Duty Station: Tanzania
Posted: 11-02-2021
No of Jobs: 1
Start Publishing: 11-02-2021
Stop Publishing (Put date of 2030): 11-02-2065
Apply Now
Notification Board

Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.

Caution: Never Pay Money in a Recruitment Process.

Some smart scams can trick you into paying for Psychometric Tests.