Rufiji Basin Water Board Chairman at Ministry of Water

Vacancy title:
Rufiji Basin Water Board Chairman

[ Type: FULL TIME , Industry: Utilities , Category: Admin & Office ]

Jobs at:

Ministry of Water

Deadline of this Job:
15 October 2021  

Duty Station:
Within Tanzania , Dodoma , East Africa

Summary
Date Posted: Monday, September 20, 2021 , Base Salary: Not Disclosed


JOB DETAILS:
Tangazo La Nafasi Ya Mwenyekiti Wa Bodi Ya Maji Ya Bonde La Rufiji
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji anatangaza nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Rufiji. Bodi hii inaundwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya mwaka 2009 chini ya Kifungu Na. 22. Muda wa Bodi ni miaka mitatu.

Majukumu Ya Bodi Ya Maji Ya Bonde La Rufiji
(a) Kuandaa mipango ya usimamizi wa rasilimali za maji, miradi, bajeti na mkakati wa utekelezaji wa Bonde;
(b) Kuunganisha mipango ya Wilaya kwenye mipango ya usimamizi wa rasilimali za maji ya Bonde:
(c) Kutoa miongozo na viwango vya ujenzi na matengenezo wa miundombinu ya vyanzo vya maji;
(d) Kufuatilia, kutathmini na kuidhinisha ujenzi na matengenezo wa miundombinu ya vyanzo vya maji:
(e) kukusanya, kuchakata na kuchambua takwimu zinazohusu usimamizi wa rasilimali za maji:
(f) Kutunza na kuboresha tathmini za upatikanaji mahitaji ya rasilimali za maji:
(g) Kuidhinisha, kutoa na kufuta vibali vya kutumia maji na kutiririsha majitaka:
(h) Kutunza Daftari la Maji kulingana na Kifungu cha 78;
(i) Kufuatilia na kutekeleza vibali vya kutumia na kutiririsha majitaka na hatua za kuzuia uchafuzi;
(j) Kutatua migogoro ndani ya Bonde;
(k) Kutekeleza miradi na programu za usimamizi wa rasilimali za maji:
(l) Kuratibu shughuli za kisekta za usimamizi wa rasilimali za maji katika ngazi ya Bonde na kuwa kiungo cha mawasiliano kati ya Sekta na watumiaji wa maji kwa ujumla;
(m) Kumshauri Mkurugenzi kwenye mambo ya kiufundi yanayohusu masuala ya maji shirikishi katika bonde;
(n) Kuteua Mwenyekiti na wajumbe wa kamati za dakio na kidakio maji; na
(o) Kutayarisha taarifa juu ya hali ya rasilimali za maji katika Bonde.

Sifa Za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa kuwa na ujuzi na uzoefu katika masuala ya Sekta ya Maji au Sekta zinazohusiana na sekta hiyo. Aidha, awe na ujuzi mahsusi kwenye masuala ya usimamizi wa rasilimali za maji na asiwel asitoke kwenye taasisi ambayo ni mtumiaji mkuu wa maji (Major Water User).

Education Requirement: No Requirements

Job Experience: No Requirements

Work Hours: 8

 

{module 312}

Job application procedure
Maombi yatumwe kwa:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Maji
Mji wa Serikali,
Mtaa wa Maji,
S.L.P. 456,
40473, DODOMA.
Nakala ya maombi itumwe kupitia barua pepe: ps@maji.go.tz

Maombi yaambatishwe na wasifu wa mwombaji (CV) yenye wadhamini watatu na namba zao za simu. Andika "Mwenyekiti Bodi ya Maji Bonde Rufiji" nyuma ya bahasha. Mwisho wa kupokea maombi ni siku ya ljumaa tarehe 15 Oktoba, 2021 saa 09.30 alasiri.


All Jobs

QUICK ALERT SUBSCRIPTION

{module 316}

Job Info
Job Category: Administrative jobs in Tanzania
Job Type: Full-time
Deadline of this Job: 15 October 2021
Duty Station: Dodoma
Posted: 20-09-2021
No of Jobs: 1
Start Publishing: 20-09-2021
Stop Publishing (Put date of 2030): 20-09-2065
Apply Now
Notification Board

Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.

Caution: Never Pay Money in a Recruitment Process.

Some smart scams can trick you into paying for Psychometric Tests.