Dereva Daraja La II Job at United Republic of Tanzania - Career Opportunity in Tanzania
Website :
1976 Days Ago
Linkedid Twitter Share on facebook

Vacancy title:
Dereva Daraja La II

Jobs at:
United Republic of Tanzania

Deadline of this Job:
7th December 2018

Duty Station:
Tanzania

Summary
Date Posted: 27th November 2018 , Base Salary: Not Disclosed , Employment Type: Full-Time

JOB DETAILS:
Jamhuri ya muungano wa tanzania ofisi ya rais sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma kumb.
Na ea.7/96/01/j/220 Tangazo la nafasi za kazi

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Maliasili na Utalii na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi za kazi 118 kama inavyooneshwa katika tangazo hili.

Bodi Ya Usajili Wa Wabunifu Majengo Na Wakadiriaji Majenzi

Dereva Daraja La II

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuendesha gari la Taasisi;
  • Kutunza na kuandika daftari la safari (log- book) kwa safari zote;
  • Kufanya uchunguzi wa gari kabla ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo;
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
  • Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote; na
  • Kutekeleza kazi nyingine yoyoye atakayopangiwa na mkuu wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Cheti cha kuhitimu Kidato cha nne (Certificate of Secondary Education), na Leseni ya Udereva Daraja “C” na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu (3) bila kusabisha ajali. Sambamba na hilo Muombaji anatakiwa kuwa na cheti cha Majarabio ya Ufundi wa Magari, Daraja la III kutoka VETA pamoja na cheti cha Udereva Mahiri Daraja la pili kutoka chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya Bodi

MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
    - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
    - Computer Certificate
    - Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 7 Desemba, 2018.
  • Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili

Job application procedure

HAYATAFIKIRIWA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/  (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

MUHIMU: KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA KAZI ILIYOSAINIWA PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU. ANUANI YA BARUA HIYO IELEKEZWE KWA
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P 63100 DAR ES SALAAM.

Job Info
Job Category: Transportation jobs in Tanzania
Job Type: Full-time
Deadline of this Job: 7th December 2018
Duty Station: Tanzania
Posted: 27-11-2018
No of Jobs: 1
Start Publishing: 27-11-2018
Stop Publishing (Put date of 2030): 27-11-2065
Apply Now
Notification Board

Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.

Caution: Never Pay Money in a Recruitment Process.

Some smart scams can trick you into paying for Psychometric Tests.