2 Village Executive III Job at Uvinza District Council - Career Opportunity in Tanzania
Website :
1589 Days Ago
Linkedid Twitter Share on facebook

Vacancy title:
2 Village Executive III

[ Type: FULL TIME , Industry: Public Administration, and Government , Category: Civil & Government ]

Jobs at:

Uvinza District Council

Deadline of this Job:
08 September 2020  

Duty Station:
Within Tanzania , Dar es Salaam , East Africa

Summary
Date Posted: Thursday, September 03, 2020 , Base Salary: Not Disclosed


JOB DETAILS:
Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi Ya Rais
Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa
Halmashauri Ya Wilaya Ya Uvinza
Kumb. Na. UDC/C20/26/I/17 26 Agosti, 2020

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi ya Mtendaji wa Kijiji III.
2 Mtendaji Wa Kijiji III .

MAJUKUMU YA KAZI:
• Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
• Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao; kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
• Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
• Katibu wa Mikutano na kamati za Halmashauri ya Kijiji.
• Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
• Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
• Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji.
• Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.
• Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalam waliopo katika Kijiji.
• Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
• Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za Kijiji; na
• Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.


Job Skills: Not Specified


SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.


MSHAHARA:
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS. B kwa mwezi.


NB: MASHARTI YA JUMLA: • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
• Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
• Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, maelezo binafsi, vyeti vya Kidato cha nne au Kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa husika na Picha moja “Passport Size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma. Viambatisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
• Kwa waombaji waliosoma nje ya nchi elimu ya Kidato cha Nne na/au Kidato cha Sita wawasilishe uthibitisho kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
• Kwa waliohitimu elimu ya chuo nje ya nchi, wawasilishe uthibitisho kutoka Baraza la Elimu ya Ufundi la Taifa (NACTE).
• Testimonials “Provisional Results” Statement of results; hati ya matokeo ya kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI Results Slip) HAVITAKUBALIWA.
• Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
• Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi; wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria.
• Uwasilishaji wa barua kwa Mkono katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza HAIRUHUSIWI.
• Waombaji wote watakaokidhi vigezo ndiyo watakaoitwa kwenye usaili (Interview).
• Maombi yasiyozingatia vigezo vilivyoainishwa katika tangazo hili hayatashughulikiwa.
• Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 08 Septemba, 2020.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza na barua ya maombi isainiwe na kuambatishwa na vielelezo vinavyohitajika na yatumwe kupitia Posta kwa anuani ifuatavyo:


Work Hours: 8

 

{module 312}

Job application procedure
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S. L. P. 12,
UVINZA.
Au

District Executive Director,
Uvinza District Council,
P. O. Box 12,
UVINZA.

NB: Tangazo hili pia linapatikana kwenye Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, www.uvinzadc.go.tz 

Arch. Weja L. Ng’olo
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA
UVINZA


All Jobs

QUICK ALERT SUBSCRIPTION

{module 316}

Job Info
Job Category: Government jobs in Tanzania
Job Type: Full-time
Deadline of this Job: 08 September 2020
Duty Station: Dar Es Salaam
Posted: 03-09-2020
No of Jobs: 2
Start Publishing: 03-09-2020
Stop Publishing (Put date of 2030): 03-09-2065
Apply Now
Notification Board

Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.

Caution: Never Pay Money in a Recruitment Process.

Some smart scams can trick you into paying for Psychometric Tests.