Vacancy title:
5 Mtendaji Wa Kijiji Daraja La III
Jobs at:
Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa
Deadline of this Job:
22nd February 2019
Summary
Date Posted: 11th January 2019 , Base Salary: Not Disclosed , Employment Type: Full-Time , Currency: Tsh
JOB DETAILS:
Ofisi Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa
Tangazo La Nafasi Za Kazi
Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa Anawatangazia Wananchi Wote Wenye Sifa Na Nia Ya Kufanya Kazi Katika Halmashauri Ya Wilaya Ya Iringa Kwa Nafasi Mbalimbali Kama Ifuatavyo;
5 Mtendaji Wa Kijiji Daraja La III
SIFA ZA MWOMBAJI:
• Awe amehitimu Kidato cha Nne au sita
• Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo:-Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
MAJUKUMU YAKE:
• Kuwa Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
• Kusimamia ulinzi na usalama wa Raia na Mali zao
• Kuratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
• Kuwa katibu wa mikutano yote ya Halmashauri ya kijiji.
• Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
• Kuandaa taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
• Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalamu katika kijiji.
• Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji.
• Mwenyekiti wa kikao cha Wataalamu waliopo katika kijiji.
• Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi.
• Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za Kijiji
• Baruapepe: ded@iringadc.go.tz
• Tovuti: www.iringadc.go.tz
• Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
NGAZI YA MSHAHARA TGS B
{module 312}
Job application procedure
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA:
• Barua za Maombi ziambatishwe na nakala za Vyeti vya Elimu, Taaluma na Cheti cha kuzaliwa,
• Mwombaji aambatishe Picha mbili za rangi(Passport Size) za hivi karibuni
• Waombaji wa nafasi ya Udereva waambatishe Leseni ya Udereva.
• Kwa wale waliosoma Nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka (TCU au NECTA kulingana na ngazi ya Cheti)
• Maombi yaambatishwe na Maelezo binafsi (CV).
• Umri wa waombaji usizidi miaka 45
• Mwisho wa kupokea maombi hayo ni tarehe 22.02.2019 saa 09:30 Alasiri.
• Barua zote za Maombi ziandikwe kwa mkono , na zitumwe kwa anuani ifuatayo;-
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya,
S. L. P. 108,
IRINGA
IMETOLEWA NA MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA.
Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.