Vacancy title:
Accountant
Â
Jobs at:
Judiciary of TanzaniaDeadline of this Job:
26th June 2019 Â
Summary
Date Posted: Tuesday, June 18, 2019 , Base Salary: Not Disclosed
JOB DETAILS:
 Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011 inaipa Tume ya Utumishi wa Mahakama jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama pamoja na majukumu yake mengine. Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapa chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Mahakama ya Tanzania katika Mikoa mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi.
Mhasibu Daraja la II TGS D – Nafasi 1.
 Sifa:-
• „Intermediate Certificate‟ inayotolewa na NBAA.
• Shahada ya Biashara/Sanaa yenye mwelekeo wa uhasibu au Stashahada ya juu ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu/ Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.
• Stashada ya Juu ya Uhasibu Serikalini (Advanced Diploma in Government Accounting) inayotolewa na Chuo cha Uhasibu kinachotambuliwa na Serikali.
Kazi za kufanya:-
• Kuidhinisha hati za malipo.
• Kuandika taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi.
• Kusimamia Wahasibu Wasaidizi katika kazi zao za kila siku.
• Kusimamia shughuli za uhasibu kwenye Kitengo cha Idara.
• Kuandika taarifa ya maduhuli
Job Skills: Not Specified
Job Education Requirements: Not Specified
Job Experience Requirements: Not Specified
Â
{module 312}
Job application procedure
 Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 26/06/2019 saa 9:30 Alasiri.
7.0 Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji na kuambatisha:-
• Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
• Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV).
• Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
• Picha mbili (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.
• Aidha, inasisitizwa kwamba:-
• Waombaji awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45 na awe hajawahi kupatikana na kosa lolote la jinai au kufungwa jela.
• Waombaji wa kazi toka maeneo husika na wenye sifa zilizoainishwa katika tangazo hili, watafikiriwa kwanza na kupangiwa kazi katika maeneo husika.
• Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi mwombaji.
• Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.
• Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.
• Waombaji watakaoshinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wawe tayari kupangiwa kwenye kituo chochote chenye nafasi wazi.
• Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE wakishindwa kutekeleza hili maombi yao hayatashughulikiwa.
• Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.
• Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha watakazotumia maombi yao.
• Waombaji waliowahi kufukuzwa kazi wasiombe.
• Waombaji wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia masharti yaliyotajwa hapo juu maombi yao hayatashughulikiwa.
• Waombaji watakaotoa taarifa za uongo mfano kuhusu umriwao, elimu yao au sehemu walizowahi kufanyia kazi na ikagundulika hata kama watakuwa wameshaajiriwa wataondolewa kazini ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
• Nakala za vyeti vya waombaji zithibitishwe na Mwanasheria
• Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391 , DAR ES SALAAM.
Imetolewa na ;-
Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391,
DAR ES SALAAM.
All Jobs
Â
Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.