Vacancy title:
Dalali wa Mahakama
Jobs at:
The United Republic Of Tanzania CourtDeadline of this Job:
19 February 2021
Summary
Date Posted: Thursday, February 11, 2021 , Base Salary: Not Disclosed
JOB DETAILS:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAHAKAMA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mahakama ya Tanzania inapenda kuutangazia umma kwamba kuna nafasi za kazi za Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama watakaofanya kazi katika Mikoa mbalimbali Tanzania Bara. Kwa mujibu wa Kanuni ya 4 na ya 6 ya Kanuni za Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama Na. 363 za Mwaka 2017(The Court Brokers and Process Servers (Appointment, Remuneration and Discipline) Rules, GN No. 363 of 2017), Kamati ya Uteuzi na Nidhamu ya Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama pamoja na majukumu mengine, imepewa jukumu la kuteua Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama wenye sifa kama zilivyoainishwa hapa chini. .
Sifa za Waombaji.
Mwombaji wa kazi ya Udalali wa Mahakama anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:-
• Raia na Mkazi wa Tanzania mwenye umri wa utu uzima.
• Mkurugenzi wa Kampuni iliyosajiliwa Tanzania au Mwendesha Mnada Mshirika katika Taasisi ambayo imesajiliwa na kupewa Leseni chini ya Sheria ya Waendesha Minada (The Auctioneers Act No. 6 Of 1928, Cap. 227).
• Awe na Elimu ya Kidato cha Nne na kuendelea na awe na uwezo kuzungumza Kingereza na Kiswahili kwa ufasaha.
• Awe amehudhuria mafunzo ya majukumu ya Madalali wa Mahakama yanayotolewa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama (IJA) na kutunukiwa Cheti cha Umahiri (Certificate of Competence).
• Awe anafahamu kikamilifu Kanuni za utekelezaji kama zilivyoainishwa na Sheria ya mwenendo wa Madai na Sheria nyingine husika.
• Awe ni mtu mwenye tabia njema na Muadilifu wa kiwango cha juu.
• Awe ni mtu mwenye msimamo mzuri wa kifedha.
• Awe na Kituo au ghala la kutosha kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa kwa ajili ya usalama.
• Awe amelipa ada ya maombi ya kiwango cha Shilingi 250,000/= ambayo haitarejeshwa.
Job Skills: Not Specified
Kazi za Kufanya.
Kutekeleza tuzo na amri za Mahakama zilizotolewa ndani ya mamlaka yake ambazo zinajumuisha:-
• Kukamata na kuuza mali za Mshindwa tuzo (Judgment Debtor). Aidha, utekelezaji huo wa amri au tuzo zinazotolewa na Mahakama lazima uzingatie Sheria ya mwenendo wa Madai na Sheria nyingine husika.
• Kutekeleza amri za kuondosha mali, vitu au watu (Eviction Orders).
• Kutekeleza amri nyingine zozote zitolewazo na Mahakama.
• Kuandaa na kuwasilisha taaarifa ya namna utekelezaji ulivyofanyika kwa Mahakama iliyotoa amri.
• Kutekeleza maelekezo mengine yoyote yatakayotolewa na Mahakama.
Ada, gharama na posho za Madalali wa Mahakama.
Ada, gharama na posho atakayolipwa Dalali wa Mahakama kutokana na kazi atakayofanya ni kama zilivyoainishwa katika Kanuni ya 27 na 28 ya Kanuni za Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka za Mahakama kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 363 la Mwaka 2017 (The Court Brokers and Process Servers (Appointment, Remuneration and Discipline) Rules, GN No. 363 of 2017).
Barua ya maombi ya Udalali wa Mahakama iambatishwe na:-
• Kivuli cha Cheti cha Elimu ya Kidato cha Nne na kuendelea.
• Kivuli cha Cheti cha Umahiri (Certificate of Competence) cha majukumu ya Dalali wa Mahakama kilichotolewa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama (IJA).
• Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV). (Taarifa isiwe na “Referees” ambaye ni ndugu, jamaa au rafiki mwenye uhusiano wa karibu na mwombaji).
• Kivuli cha Cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha Uraia.
• Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.
• Barua ya utambulisho ya Benki kuhusu Akaunti ya Mwombaji.
• Fomu ya Maombi ya Udalali (Fomu Na. 3) iliyojazwa kikamilifu.
• (Fomu ya Wadhamini wawili wa Muombaji (Fomu Na. 5) yenye jumla ya kiwango cha udhamini kisichopungua Milioni mia nne (400,000,000/=).
• Leseni ya Biashara kutoka katika Halmashauri ya Jiji, Mji au Manispaa.
• Barua ya utambulisho juu ya tabia ya Mwombaji kutoka kwa watu wanaoaminiwa. (Barua isiandikwe na ndugu, jamaa au rafiki mwenye uhusiano wa karibu na mwombaji).
• Nakala ya hati ya Bima ya moto, majanga na wizi ambayo ni hai kwa mujibu wa Sheria au ahadi ya maandishi ya kukata Bima hiyo baada ya kuteuliwa kuwa Dalali wa Mahakama.
• Nakala ya Cheti cha usajili wa Kampuni ambayo Mwombaji ataitumia katika kazi ya Udalali wa Mahakama au Leseni ya Udalali wa Kawaida (Auctioneers’ General License).
• MEMART (Memorandum and Articles of Association) ya Kampuni itakayotumika katika kazi ya Udalali.
• Nakala ya uthibitisho wa malipo ya Kodi (TIN).
• Taarifa ya Benki ya miezi kumi na miwili (12) ya hivi karibuni inayoonesha uwezo wa Kifedha wa Kampuni itakayotumika au uwezo wa Mwombaji.
• Hati ya kubadilisha jina (Deed Poll) iwapo kuna tofauti ya majina katika nyaraka zitakazotumika katika maombi ya Mwombaji.
• Uthibitisho wa umiliki wa Ofisi, yadi na ghala la kuhifadhia bidhaa au mkataba wa upangishaji.
Work Hours: 8
{module 312}
Job application procedure
Fomu zote za maombi ya Udalali wa Mahakama na Wadhamini wake na Wasambaza Nyaraka za Mahakama zinapatikana katika Ofisi zote za Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi (Mkoa) Tanzania Bara na Ofisi ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, DAR ES SALAAM.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 19/02/2021 saa 9:30 alasiri.
Mwombaji wa nafasi ya Dalali wa Mahakama na Msambaza Nyaraka za Mahakama aandaye nakala tatu (3) na atume maombi yake kwa njia ya Posta (E.M.S) au kwa Mkono na kuwasilishwa kwa Msajili, Mahakama Kuu, S.L.P 9004, DAR ES SALAAM.
Imetolewa leo tarehe 04 Februari 2021 na:-
M.J. Chaba
Kny: MSAJILI
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA
All Jobs
{module 316}
Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.