Vacancy title:
Katibu Muhtasi III
Jobs at:
Tandahimba District CouncilDeadline of this Job:
08 February 2021 Â
Summary
Date Posted: Thursday, January 28, 2021 , Base Salary: Not Disclosed
JOB DETAILS:
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Tandahimba anawatangazia waombaji wote ya kazi kwa nafasi ziliyoainishwa hapa chini, baada ya kupata kibali cha ajira mbadala chenye Kumb. Na FA. 170/362/01/"A"/114 cha tarehe 15 Disemba 2020, kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu ajira mpya. Hivyo basi Mkurugenzi Mtendaji (W) Tandahimba anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa .
Sifa za Kitaaluma za Mwombaji.
• Awe na Elimu ya Kidato cha Nne
• Awe amehudhuria mafunzo ya Uhazili na kufaulu mitihani ya hatua ya tatu.
• Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja.
• Awe amepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika Progamu za Windows, Microsoft Office, internet, E-mail na Publisher.
Mshahara
Katibu Muhtasi Il ataanza na mshahara wa TGS B1 kwa mwezi, kulingana na viwango vya Serikali vya nafasi hiyo
Majukumu ya Katibu Muhtasi III
• Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
• Kusaidia kupokea wageni, na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
• Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miradi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
• Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka, au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi Ofisini.
• Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kuhusu taarifa zozote atakazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
• Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maofisa waliopo katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
• Kutekeleza shughuli zozote atakazokuwa amepangiwa na mkuu wake w kazi.
Job Education Requirements: Not Specified
Job Education Experience: Not Specified
Work Hours: 8
Â
{module 312}
Job application procedure
MASHARTI YA JUMLA YA MWOMBAJI WA NAFASI ZA KAZI
• Awe raia wa Tanzania.
• Awe na miaka kuanzia 18 hadi 45.
• Mwombaji mwenye cheti cha kughushi asijaribu kuomba nafasi hizi, endapo atabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
• Awe hajawahi kufukuzwa kazi, kupunguzwa, kuachishwa kazi au kustaafishwa kazi katika Utumishi wa Umma.
• Awe tayari kufanya kazi katika kijiji chochote kile ndani ya Halmashauri ya Wilaya Tandahimba.
• Waombaji waambatanishe vivuli vya vyeti vyao vya shule, taaluma, kuzaliwa. • Curriculum Vitae (CV)
• Taarifa binafsi za mwombaji
• Kila mwombaji aambatanishe na picha ndogo 2 passport size zilizopigwa hivi karibuni.
• Kila mwombaji aandike kwa usahihi anwani yake, na namba ya simu inayopatikana muda wote.
NUKUU: Maombi yote yatumwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji (W),
S.L.P. 03,
TANDAHIMBA - MTWARA.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 08 Feburari, 2021 saa 9.30 Alasiri.
All Jobs
{module 316}
Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.