Vacancy title:
Mtendaji Wa Kijiji Daraja La III
Jobs at:
Mbinga Town CouncilDeadline of this Job:
22 October 2020
Summary
Date Posted: Tuesday, October 13, 2020 , Base Salary: Not Disclosed
JOB DETAILS:
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
UTANGULIZI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga baada ya kupokea kibali cha ajira Mbadala chenye Kumb Na. FA.170/367/01"A"/ cha tarehe 5 Agosti, 2020 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Na Utawala Bora, anawatangazia wananchi wote Raia wa Tanzania wenye sifa zinazohitajika kuomba nafasi wazi Mbili (2) kama zifuatazo: .
KAZI NA MAJUKUMU
• Afisa masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
• Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika kijiji.
• Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
• Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji y.
• Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na taratibu.
• Kuandaa Taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mkakati wa kuondoa Njaa, Umaskini na kuongeza Uzalishaji Mali
• Kiongozi wa wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji
• Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyara Kijiji
• Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalamu waliopo Katika Kijiji
• Kupokea, Kusikiliza na kutatua malalamiko ya Migogoro ya Wananchi
• Kusimamia utungaji wa Sheria ndogo za kijiji na
• Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
Job Skills: Not Specified
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa waliohitimu kidato cha nne au cha sita na waliohudhuria mafunzo ya Astashahada/Cheti NTA LEVEL 5 katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Sayansi ya jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya jamii na Sayansi ya Jamii kutoka Chuo cha serikali za mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambulika na serikali.
Job Education Requirements: Not Specified
MSHAHARA Kwa kuzingatia Viwango vya Mishahara ya Serikali Ngazi ya Mshahara itakuwa TGS B.
Work Hours: 8
{module 312}
Job application procedure
MAELEZO/ MASHARTI YA JUMLA
• Mwombaji awe raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya Miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18
• Barua iambatanishwe na Wasifu binafsi wa mwombaji wa hivi karibuni (Curriculum Vitae) anuani inayotumika, namba ya simu na anuani ya barua pepe (e-mail address) na majina ya wadhamini (referees) watatu wanaofahamika.
• Waombaji lazima waambatanishe nakala za vyeti vifuatavyo vili
• onyeshwa kwenye nafasi aliyoomba:- Mfano
a) Astashahada/cheti cha utaalamu kulingana na sifa za nafasi husika
b) Cheti cha kidato cha nne au sita
c) Cheti cha kuzaliwa
• Matokeo ya muda (provisional/testimonials/statement of results) havitakubaliwa.
• Waombaji wawe wenye sifa na uzoefu uliotajwa kwenye tangazo hili la kazi
• Picha 2 ndogo (passport size) za hivi karibuni.waombaji watakaoleta maombi na vyeti vya kugushi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao
• Waombaji wa makundi maalum wanashawishiwa kuomba
• Waombaji wenye vyeti vya kidato cha nne na sita vya nje ya nchi vitatakiwa vithibitishwe na NACTE.
• Waombaji wenye vyeti vya Astashahada na Diploma vya nje ya nchi vithibitishwe na NACTE. • Barua ya muombaji itatakiwa iandikwe kwa Kiswahili au kiingereza
• Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta.
• Barua zitakazoletwa mkononi hazitapokelewa wala kufanyiwa kazi.
• Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 22/10/2020 Saa 9:30 Alasiri. Maombi yote yatumwe kwa:
Mkurugenzi wa Mji,
Halmashauri ya Mji wa Mbinga,
S. L. P. 135,
MBINGA
All Jobs
{module 316}
Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.