Vacancy title:
2 Mhasibu Msaidizi
Jobs at:
Halmashauri Ya Wilaya Ya Chemba
Deadline of this Job:
15th April 2019
Summary
Date Posted: 8th April 2019 , Base Salary: Not Disclosed , Employment Type: Full_Time , Currency: TZS , Value: 625000 , Minimum: 437500 , Maximum: 1875000 , Period: MONTH
JOB DETAILS:
Halmashauri Ya Wilaya Ya Chemba (Barua zote zitumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji) 02/04/2019
Kumb. Na. CDC/LGA/A/5/5
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI (INTERNAL RECRUITMENT)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Kupitia Mwongozo wa bajeti wa mwaka 2019/2020 kutoka kwa Katibu Mkuu ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, umeelekeza waajiri kujaza nafasi wazi kwa kutumia rasilimali watu waliopo kwenye taasisi husika waliojiendeleza katika fani yenye upungufu na uhitaji.
kupitia tangazo hili, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji inapenda kuwatangazia watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba wenye sifa za kimuundo kutuma maombi ya kazi zilizoainishwa hapa chini.
2 Mhasibu Msaidizi – (ngazi ya mshahara TGS C1=525,000).
Sifa za kuajiriwa/kubadilishwa muundo kwa waliopo kazini:
• Awe na mwenye cheti cha kufaulu mtihani mgumu wa uhasibu Serikalini (Higher Standard Government Accountancy Examination) unaotolewa na Tume ya Utumishi wa Umma.
• Awe na Stashahada ya kawaida ya uhasibu kutoka chuo/Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.
Kazi za kufanya.
• Kupokea na kulipa fedha.
• kutunza daftari la fedha.
• Kufanya usuluhisho wa hesabu za benki.
• Kukagua hati za malipo..
{module 312}
Job application procedure
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
Maombi yapitishwe na msimamizi wa kituo cha kazi pamoja na mkuu wa idara yako na yatumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji
• Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, S.L.P. 830, Chemba.
• Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15/04/2019 saa 9:30 Alasiri.
• Waombaji watakaokidhi vigezo wataandikiwa barua ya moja kwa moja kuripoti ofisi ya Mkurugenzi tayari kwa kuanza kutekeleza majukumu mapya na wawe tayari kujigharamia kuhamia makao makuu ya Halmashauri.
• Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma na ujuzi.
• Waombaji watakaokidhi vigezo wawe tayari kubadilishwa muundo wa utumishi na ngazi ya mshahara kulingana na Sera ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Entry point).
• Muombaji ambaye hataandikiwa barua ya wito, atambue kwamba hajakidhi vigezo au maombi yake yamechelewa.
• Awe ni mwajiriwa katika masharti ya kudumu katika Utumishi wa Umma.
MKURUGE ZI MTENDAJI WILAYA YA CHEMBA
Dkt. Semistatus 'H. Mashimba
MKURUGENZI MTENDAJI. HALMASHAURI YA WILAYA,
CHEMBA.
Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.