4 Village Executives Jobs at Sengerema District Council - Career Opportunity in Tanzania
1182 Days Ago
Linkedid Twitter Share on facebook

Vacancy title:
4 Village Executives

[ Type: FULL TIME , Industry: Public Administration, and Government , Category: Civil & Government ]

Jobs at:

Sengerema District Council

Deadline of this Job:
13 September 2021  

Duty Station:
Within Tanzania , Sengerema , East Africa

Summary
Date Posted: Friday, August 27, 2021 , Base Salary: Not Disclosed


JOB DETAILS:
Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Ofisi Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa Halmashauri Ya Wilaya Ya Sengerema
Kumb. Na. AB.16/194/02/175

Tangazo La Nafasi Za Kazi Mkurugenzi Mendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema alipokea kibali cha ajira mbadala kwa Watendaji wa Vijiji Ill nafasi (04) kwa kibali chenye kumb. Na. FA.170/359/01/"A"/125 ya tarehe 29 Julai, 2021 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi za kazi 04 kama zilizoainishwa katika tangazo hili
Mtendaji Wa Kijiji (Village Executive) Daraja La Iii - Nafasi (04)

Majukumu Ya Kazi
• Mtendaji na mshauri wa Halmashauri ya Kijiji na Kamati zake katika mipango ya maendeleo ya kijamii na utekelezaji wa mipango ya maendeleo
• Afisa masuhuli na mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na matumizi ya Halmashauri ya Kijiji.
• Mlinzi wa amani na msimamizi wa Utawala Bora katika Kijui
• Kuratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji
• Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji
• Kutafsiri Sera, Utaratibu na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo za Halmashauri katika Kijiji.
• Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika kijiji chake na kuziwasilisha kwenye Kata
• Kuongoza vikao vya maendeleo ya Kijiji vitakavyohusisha wananchi na wataalam waliopo kwenye eneo lake.
• Kuhamasisha wananchi katika mikakati mbalimbali ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji
• Kusimamia matumizi bora ya nguvu kazi.
• Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo wa kitaalamu katika kijiji

Sifa za Mwombaji
• Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha nne au sita aliyehitimu mafunzo Astashahada/cheti NTA LEVEL 5 katika moja ya fani zifuatazo:- Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa katika chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo- Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Mshahara
• Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali

TGS B Masharti Ya Mwombaji
• Mwombaji anatakiwa awe Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi mika 45
• Mwombaji aambatishe cheti cha kuzaliwa
• Mwombaji ambaye tayari ni Mtumishi wa Umma na amejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na alizonazo, apitishe barua yake ya maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wake.
• Mwombaji aambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu zinazopatikana pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
• Maombi yote yaambatishwe na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya Kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
i) Certificates
ii) Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
iii) Computer Certificate
iv) Vyeti vya kitaaluma (Professional certificate from respective boards)
v) Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni.
• Testmonial", "Provisional Results", "Statement of Results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA

Mwombaji aliyesoma nje ya Tanzania ahakikishe vyeti vyake vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).
Mwombaji wa nafasi ya Ajira aliyestaafishwa/kuachishwa kazi katika Utumishi wa Umma haruhusiwi kuomba isipokuwa kama anakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
Mwombaji wa kazi ambaye tayari ni mwajiriwa katika nafasi ya kuingilia aliyeko katika Utumishi wa Umma asiombe kwa kuzingati maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010

Job Experience: No Requirements

Work Hours: 8


Level of Education:
Professional Certificate

 

{module 312}

Job application procedure
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachuliwa hatua za sheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 13 Septemba 2021 saa 9.30 Alasiri. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu uliobainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya Posta kupitia anuani ifuatayo:

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema
S.L.P.175,
SENGEREMA.

Binuru M. Shekidele
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Sengerema.


All Jobs

QUICK ALERT SUBSCRIPTION

{module 316}

Job Info
Job Category: Government jobs in Tanzania
Job Type: Full-time
Deadline of this Job: 13 September 2021
Duty Station: Sengerema
Posted: 27-08-2021
No of Jobs: 4
Start Publishing: 27-08-2021
Stop Publishing (Put date of 2030): 27-08-2065
Apply Now
Notification Board

Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.

Caution: Never Pay Money in a Recruitment Process.

Some smart scams can trick you into paying for Psychometric Tests.