4 Wataalamu wa Tiba Liwaza Jobs at Sense International Tanzania - Career Opportunity in Tanzania
Website :
2206 Days Ago
Linkedid Twitter Share on facebook

Vacancy title:
4 Wataalamu wa Tiba Liwaza

Jobs at:
Sense International Tanzania

Deadline of this Job:
12th November 2018

Duty Station:
Tanzania

Summary
Date Posted: 8th November 2018 , Base Salary: Not Disclosed , Employment Type: Full-Time

Sense International ni shirika lisilo la kiserikali linalofanya shughuli za kuhudumia jamii ya watu wenye ulemavu wa uziwikutoona (Deafblindness) ili waweze kujifunza,kuishi na kufanikiwa. Aidha,shughuli za shirika zipo nchini Bangladesh, India, Nepal, Tanzania, Peru, Romania na Uganda. Nchini Tanzania, Sense International inashirikiana na serikali na asasi mbalimbali katika kuwatambua watu wenye uziwikutoona kisha kuwawezesha kielimu, kiafya na namna ya kujikimu kimaisha ili waweze kushiriki na kuchangia maendeleo ya jamii. Ili kuhakikisha ya kwamba mabadiliko ya utoaji huduma yanakuwa endelevu shirika linawekeza katika kufanya ushawishi wa mabadiliko ya sera ili ziakisi utoaji wa huduma kulingana na mahitaji ya watu wenye ulemavu, kujenga mazingira wezeshi ya utoaji wa huduma za elimu na afya kwa watu wenye uziwikutoona pamoja na kuwaendeleza na kuwatumia wataalamu wazawa.

JOB DETAILS:
Hivi sasa Sense International Tanzania kwa kushirikiana na Manispaa ya Temeke inahitaji wataalamu wa Tiba liwaza (Occupational Therapist) kwa ajili ya kufanya kazi katika mradi wa kufanya Utambuzi na utoaji wa Afua za Mapema (Early Intervention) kwa watoto wenye uziwikutoona na wenye ulemavu mwingine mchanganyiko kuanzia miaka 0-5. Mradi huu ni wa ufadhili wa Jessey Overseas Aid (JOA) kutoka nchini Uingereza.

Wataalamu wa Tiba Liwaza
Wilaya: Temeke
Mkoa: Dar es Salaam
Muda wa ajira: Miaka 2 au zaidi kutegemeana na uwepo wa ufadhili.
Mshahara: Mshahara mzuri sambamba na marupurupu.

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuwezesha na kufanya ubaini kama mtoto anafaa kupatiwa Afua za Mapema (Early Intervention services).
  • Kutoa msaada wa kitaalamu wa jinsi ya kuwahudumia watoto wenye uziwikutoona na wale wenye ulemavu mwingine mchanganyiko katika kukabiliana na changamoto za mawasiliano na kujimudu kwa kutumia mtaala ulioandaliwa.
  • Kutoa ushauri kuhusu changamoto mbalimbali katika utumiaji wa vifaa vinavyotumika kuwasaidia watoto wenye uziwikutoona.
  • Kushirikiana na madaktari, wataalamu wa tiba viungo, maafisa ustawi wa jamii na wauguzi katika ngazi ya jamii pamoja na familia za watoto wenye uziwikutoona katika mlengo wa kusadia maendeleo ya watoto wenye uziwikutoona.
  • Kusimamia uendeshaji wa kituo cha kufanya utambuzi na utoaji wa Afua za Mapema (Early Intervention unit).
  • Kutunza siri na umakini wa taarifa za watoto wanaohudumiwa kituoni kwa kutumia mifumo ya analojia na digitali itakayokuwepo kituoni.
  • Kuandaa taarifa za wiki na mwezi ili kuzituma kwa mamlaka husika katika kituo cha Afya na Sense International Tanzania.
  • Kushiriki katika kuelimisha jamii kuhusu huduma ya upimaji na usaidizi wa awali katika kituo cha kutolea huduma, katika jamii na mahali pengine utakapohitajika.

Tunatafuta mtaalamu wa tiba liwaza mwenye uzoefu katika kazi yake, mwenye uwezo wa kuhudumia watu kwa weledi, kuwasiliana vizuri na kutoa taarifa ya maendeleo kwa umakini.

VIGEZO VYA MWOMBAJI:

  • Awe na “Diploma”ya Tiba Liwaza (Occupational Therapy) kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
  • Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili.
  • Uzoefu wa kudumia watoto wenye ulemavu hususani wenye uziwi-kutoona (Deafblindness).

Kufahamu zaidi kuhusu kazi zetu, tembelea: https://www.senseinternational.org.uk/our-work/tanzania

Job application procedure
Kama una vigezo stahiki na ungependa kuomba kazi hii, tuma barua yako ya maombi na wasifu wako kwa Mkurugezi, Sense International Tanzania, P O BOX 82653, Dar es Salaam kupitia infotz@senseint-ea.org . Unapotuma barua pepe, weka kichwa (SUBJECT) MTAALAMU TIBA LIWAZA – TANZANIA. Tafadhali elezea kwenye barua yako ya maombi sababu za kupendezwa na nafasi hii, ni kwa jinsi gani ujuzi na uzoefu wako unashabihiana na kazi hii, pia elezea mshahara unaopokea sasa pamoja na namba yako ya simu inayopatikana. Mwisho wa kutuma maombi ni saa 11 kamili jioni, tarehe 12 Novemba, 2018. Ni wale tu waliofuzu ndio watapokea majibu. Sense International inaajiri bila kuzingatia jinsia, dini, rangi, kabila, uraia,hali ya ulemavu au namna yoyote ya ubaguzi.

Job Info
Job Category: NGO - Non Government Organisations jobs in Tanzania
Job Type: Full-time
Deadline of this Job: 12th November 2018
Duty Station: Tanzania
Posted: 08-11-2018
No of Jobs: 4
Start Publishing: 08-11-2018
Stop Publishing (Put date of 2030): 08-11-2065
Apply Now
Notification Board

Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.

Caution: Never Pay Money in a Recruitment Process.

Some smart scams can trick you into paying for Psychometric Tests.