41 Mhifadhi Wanyamapori Daraja la III Jobs at Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Career Opportunity in Tanzania
Website :
2170 Days Ago
Linkedid Twitter Share on facebook

Vacancy title:
41 Mhifadhi Wanyamapori Daraja la III

Jobs at:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Deadline of this Job:
26th December 2018

Duty Station:
Tanzania

Summary
Date Posted: 13th December 2018 , Base Salary: Not Disclosed , Employment Type: Full-Time

JOB DETAILS:
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Kumb. Na EA.7/96/01/J/232 12 Desemba, 2018

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 41 kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.

Mhifadhi Wanyamapori Daraja la III

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi;
  • Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi;
  • Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha;
  • Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori;
  • Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali;
  • Kufanya usafi na ulinzi wa kambi;
  • Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi;
  • Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani;
  • Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kukusanya takwimu zao;
  •  Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya Nchi;
  • Kudhibiti wanyamapori waharibifu;
  • Kudhibiti moto kwenye hifadhi, na
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya Uhifadhi Wanyamapori (Technician Certificate in Wildlife Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B2

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE.

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa wale tu ambao wapo ndani ya utumishi wa Umma.
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
    - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
    - Computer Certificate
    - Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
    - Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
  • Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  •  Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 26 Desemba, 2018.
  • Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
    HAYATAFIKIRIWA

Job application procedure
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/  (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

MUHIMU: KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA KAZI
ILIYOSAINIWA PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU KWA LUGHA YA KISWAHILI AU KIINGEREZA.

ANUANI YA BARUA HIYO IELEKEZWE KWA:
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P 63100 DAR ES SALAAM AU

KWA KIINGEREZA KWA ANUANI HII:
SECRETARY, PRESIDENT’S OFFICE, PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT, 27 BIBITITI MOHAMMED ROAD, P.O. BOX 63100, MAKTABA COMPLEX, 11102 DAR ESSALAAM IMETOLEWA NA KATIBU, SEKRETATARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMA

Job Info
Job Category: Government jobs in Tanzania
Job Type: Full-time
Deadline of this Job: 26th December 2018
Duty Station: Tanzania
Posted: 13-12-2018
No of Jobs: 41
Start Publishing: 13-12-2018
Stop Publishing (Put date of 2030): 13-12-2065
Apply Now
Notification Board

Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.

Caution: Never Pay Money in a Recruitment Process.

Some smart scams can trick you into paying for Psychometric Tests.