5 Mkaguzi Wa Ndani II – (Internal Auditor II) Job at Judicial Service Commission - Career Opportunity in Tanzania
Website :
497 Days Ago
Linkedid Twitter Share on facebook

Vacancy title:
5 Mkaguzi Wa Ndani II – (Internal Auditor II)

[ Type: FULL TIME , Industry: Public Administration, and Government , Category: Accounting & Finance ]

Jobs at:

Judicial Service Commission

Deadline of this Job:
01 March 2021  

Duty Station:
Within Tanzania , Dar es Salaam , East Africa

Summary
Date Posted: Thursday, February 18, 2021 , Base Salary: Not Disclosed


JOB DETAILS:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 35
Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa Ibara ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011 inaipa Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na majukumu yake mengine, mamlaka ya kuajiri watumishi wa Mahakama wa kada mbalimbali.
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapa chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Mahakama ya Tanzania katika Mikoa na Wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi. Nafasi hizo ni Afisa Tehama II - (TGS E) nafasi 10, Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani II - (TGS E) nafasi 5, Afisa Ugavi II - (TGS D) nafasi 5, Afisa Ugavi Msaidizi – (TGS C) nafasi 3, Opereta wa Kompyuta Msaidizi – (TGS B) nafasi 1, Mpokezi (TGS B) nafasi 1, na Dereva II – (TGS B) nafasi 10. .

Kazi za kufanya:-
• Kuandaa program ya ukaguzi wa ndani.
• Kufanya uchambuzi katika hatua za awali za ukaguzi.
• Kufanya tathmini za udhibiti wa mifumo ya ndani katika hatua za awali (Internal Controls), udhibiti wa vihatarishi (Risk management) na usimamizi wa mifumo ya uendeshaji (corporate governance)
• Kuandaa mpango wa ukaguzi wa ndani wa kawaida au Maalum.
• Kufanya ukaguzi wa kawaida, Maalum, kiufundi na uchunguzi (Normal, Special audit, Technical Audit and Investigations).
• Kufanya uhakiki wa hoja za ukaguzi zilizopokelewa.
• Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi wa Ndani.
• Kutoa ushauri wa kuimarisha utendaji wa Taasisi
Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.


Job Skills: Not Specified


Sifa:-
Waombaji wawe na Shahada ya Biashara au Sanaa yenye mwelekeo wa Uhasibu/Stashahada ya Juu ya Uhasibu/Ukaguzi Hesabu wenye cheti cha Taaluma ya Uhasibu CPA (T) au sifa nyingine zinazotambulika na NBAA.


Job Education Requirements: Not Specified


Job Education Experience: Not Specified


Work Hours: 8

 

{module 312}

Job application procedure
Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 1/3/2021 saa 9:30 Alasiri.
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi pamoja na namba ya simu na kuambatisha:-
- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
- Wasifu wa mwombaji (CV).
- Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
- Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni ambazo zimeandikwa majina nyuma yake .
NB. Nakala za vyeti vya taaluma na vya kidato cha nne/sita vithibitishwe na Hakimu/Wakili anayetambuliwa na Serikali (True copies of the originals).
• Aidha, inasisitizwa kwamba:-
• Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44.
• Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi mwombaji.
• Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.
• Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.
• Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wawe tayari kufanya kazi katika mikoa na Wilaya mbalimbali za Tanzania bara.
• Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE.
• Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.
• Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha watakazotumia maombi yao.
• Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma.
• Waombaji ambao wataficha ama kutoonyesha kwenye viambatisho vyao sifa yoyote ya kielimu waliyonayo na ikabainika wakati wa mchakato wa kuwaajiri mchakato huo utasitishwa na hata kama watakuwa tayari wameajiriwa, ajira zao zitasitishwa mara moja.
• Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi moja.
• Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao hayatashughulikiwa.
• Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu,
• Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391,
DAR ES SALAAM.
Imetolewa na ;-
Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P 8391,
DAR ES SALAAM,


All Jobs

QUICK ALERT SUBSCRIPTION

{module 316}

Job Info
Job Category: Accounting/ Finance jobs in Tanzania
Job Type: Full-time
Deadline of this Job: 01 March 2021
Duty Station: Tanzania
Posted: 18-02-2021
No of Jobs: 5
Start Publishing: 18-02-2021
Stop Publishing (Put date of 2030): 18-02-2065
Apply Now

Notification Board:

Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.

Caution: Never Pay Money in a Recruitment Process.

Some smart scams can trick you into paying for Psychometric Tests.