Job Vacancies at The United African University Of Tanzania
Website :
529 Days Ago
Linkedid Twitter Share on facebook

Meneja Mkuu:

Madhumuni ya kazi: ni kuongeza ufanisi wa kazi katika upangaji, uratibu na usimamizi shughuli za Kampuni ikiwa ni pamoja na kuongeza Masoko na kuweka mifumo ya uthibiti wa mapato katika vyanzo vyote vya kampuni.

Atawajibika kwa Mkurugenzi Mtendaji.

Majukumu makuu yatakuwa yafuatayo:-

a) Kumshauri Mkurugenzi Mtendaji, Board ya Wakurugenzi na uongozi juu ya mikakakati sahihi ya kuongeza mauzo ya Kampuni, kuimarisha tija kwa kuzingatia (compliance) sheria mbalimbali na taratibu za uendeshaji wa Makapuni na uthibiti (Regulatory framework).

b) Kama msimamizi mkuu wa Shughuli za Kampuni kuhakikisha kumbukumbu zote muhimu na taarifa mbalimbali za uendeshaji zinaandaliwa na kuwasilishwa panapo husika kwa muda.

c) Kama kiongozi mkuu wa wafanyakazi wa kampuni walioko kwenye Idara mbali mbali kuhakikisha matakwa yote ya kisheria na uthibiti(regulatory Authorities) yanazingatiwa. d) Kuandaa na kusimamia Bajeti za kampuni za muda mfupi na mrefu kwenye masuala ya Mapato na Matumizi. e) Kuratibu utendaji wa pamoja (Team work) katika ushirikiano wa malengo ya kazi kwa Idara zote. f) Kuweka mfumo wa mawasiliano, kukusanya taarifa za kibishara na masoko, kuandaa taarifa za utendaji na kusimamia maamuzi ya Vikao na Maelekezo ya Board ya Wakurugenzi na kuhakikisha yanatekelezeka kwa muda. g) Kutambua viashiria vya athari kuu (key risks) za kibishara na kuweka mikakati ya kuzipunguza au kuziepuka kabisa kwa kuzingatia maslahi ya Kampuni.

h) Kutafiti na kufungua Masoko Mapya na kuendeleza yaliyopo, kushauri juu ya mikakati sahihi ya kuongeza mauzo na tija kwenye kampuni soko.

i) Kutathmini utendaji wa watumishi walio chini yako na kushauri uongozi hatua stahiki za kuchukua ili kuboresha utendaji wao na tija kwa ujumla.

Sifa na uzoefu wa Mwombaji:

Mwombaji wa nafasi ya Meneja Mkuu sharti awe na sifa zifuatazo:-

.

Shahada ya kwanza ya elimu ya biashara au Masoko Shahada ya uzamili katika fani hiyo au uongozi wa biashara itakuwa ni faida ya ziada.

Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitano katika nafasi ya juu kama hii katika Kampuni ya Kibiashara iliyopata mafanikio.

Awe na uwezo mzuri wa kuwasiliana na wateja na wadau wengine wa kikazi, kujenga na kuwasilisha hoja pamoja na kujenga mahusiano mazuri nao.

Awe na uwezo wa kuongoza na kusimamia wenzie, mbunifu, mchambuzi na mwenye kiu ya mafanikio ya kitaasisi.

Mtunza Stoo:

Mtunza stoo atakuwa ndiye msimamizi mkuu wa Stoo na atawajibika kuhakikisha usalama wa mali zote zilizopo humo. Atawajibika moja kwa moja kwa Mhasibu Mkuu.

b)

Majukumu ya Mtunzaji wa Stoo yatakuwa kama ifuatavyo: a) Kusimamia shughuli zote za uanzishaji wa mchakato wa uagizaji bidhaa, upokeaji na utoaji wa bidhaa stoo/ghalani Kuandaa na kutunza kumbukumbu zote na taarifa za kila siku, wiki, mwezi na mwaka juu ya bidhaa zilizopokelewa na zilizotolewa ghalani na zilizopo (Stock Inventory). c) Kusimamia shughuli zote za upangaji wa bidhaa zilizomo ghalani kwa kuhakikisha kunakuwa na nafasi ya kupokelea bidhaa wakati wowote.

d) Kuhakikisha bidhaa zote zitolewazo ghalani zinafuata mfumo maalum uliowekwa na Kampuni ili kuepuka uharibifu au upotevu wa bidhaa na uagizaji wa bidhaa holela.

e) Kuchunguza viashiria hatarishi na kutoa taarifa mapema kwa uongozi juu ya uzuiaji wake.

Sifa za Mwombaji:

Mwombaji wa nafasi hii sharti awe na sifa zifuatazo:

Elimu ya Stashahada au Shahada katika fani ya Ugavi (supplies au utunzaji wa bidhaa (matrials Mnagement). Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili kwenye shughuli za usimamizi wa stoo/Ghala.

Kama una amini una vigezo vyote vya nafasi husika hapo juu tafadhali wasilisha maombi yako kupitia Anuani ifuatayo: Mkurugenzi Mtendaji, M/S: J.K (2005) Limited,

S.L.P 10497, Mwanza

au

kupitia Barua pepe jk2005ltd@yahoo.com.

Mwisho wa kupokea maombi ni siku Ishirini tangu tarehe ya tangazo. Watakao kidhi vigezo tu ndiyo watakaoitwa kwenye usaili.

Job Info
Job Category: Accounting/ Finance jobs in Tanzania
Job Type: Full-time
Deadline of this Job: 18 January 2023
Duty Station: Dar es Salaam
Posted: 02-01-2023
No of Jobs: 1
Start Publishing: 03-01-2023
Stop Publishing (Put date of 2030): 02-01-2077
Apply Now
Notification Board

Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.

Caution: Never Pay Money in a Recruitment Process.

Some smart scams can trick you into paying for Psychometric Tests.