Mtendaji Wa Kijiji III Job at Itilima District Council - Career Opportunity in Tanzania
Website :
1609 Days Ago
Linkedid Twitter Share on facebook

Vacancy title:
Mtendaji Wa Kijiji III

[ Type: FULL TIME , Industry: Public Administration, and Government , Category: Civil & Government ]

Jobs at:

Itilima District Council

Deadline of this Job:
19 August 2020  

Duty Station:
Within Tanzania , Itilima , East Africa

Summary
Date Posted: Friday, August 14, 2020 , Base Salary: Not Disclosed


JOB DETAILS:
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi ya Mtendaji wa Kijiji III. Tangazo hili limetokana na kibali cha Ajira Mbadala chenye Kumb.Na FA. 171533/01/"A"/122 cha tarehe 30/06/2020 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. .

MAJUKUMU
• Afisa Masuuli (Mhasibu) na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
• Kusimamia ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika kijiji.
• Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji. Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya kijiji.
• Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
• Kuandaa Taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali.
• Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaalum katika Kijiji.
• Kusimamia ukusanyaji na kuhifadhi kumbukumbu zote za nyaraka za Kijiji.
• Mwenyekiti wa kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji.
• Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
• Kusimamia utungaji wa sheria Ndogo za Kijiji na
• Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata


Job Skills: Not Specified


SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu wa Kidato cha IV au VI aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika mojawapo wa fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Jamii kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo,Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.


Job Education Requirements: Not Specified


MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za Mishahara ya Serikali TGS.B


Work Hours: 8

 

{module 312}

Job application procedure
MASHARTI YA JUMLA
• Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 hadi 45.
• Muombaji awasilishe picha moja ya hivi karibuni.
• Waombaji wawasilishe Maelezo binafsi yanayojitosheleza(Detailed CV) yenye anuani na namba za simu pamoja na majina ya wadhamini watatu (Referees) na namba zao za simu.
• Waombaji wote waambatanishe nakala ya vyeti halisi vya masomo na taaluma (NTA level 5) transcript ya cheti cha taaluma na cheti cha kuzaliwa. Muombaji atakayewasilisha"Result slip" "statement of results","Provisional results au "Transcript" bila nakala halisi ya cheti cha taaluma maombi yake hayatakubaliwa.
• Kwa waliosoma nje ya nchi elimu ya kidato cha nne na kidato cha sita wawasilishe uthibitisho kutoka Baraza la Mitahani la Tanzania (NECTA).
• Kwa waliomaliza vyuo nje ya nchi wawasilishe uthibitisho kutoka Baraza la Elimu ya Ufundi la Taifa (NACTE).
• Wote watakaokidhi vigezo ndio watakaoitwa kwenye usaili (Interview).
• Maombi yasiyozingatia vigezo vilivyoainishwa hayatashughulikiwa.
• Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 19/08/2020 saa 9:30 Alasiri.

MUHIMU:Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vielelezo vyote vilivyohitajika. Maombi yote yatumwe Kwa:
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA,
S.L.P. 308
ITILIMA.
Tangazo hili pia linapatikana kwenye Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima www.itilimadc.go.tz


All Jobs

QUICK ALERT SUBSCRIPTION

{module 316}

Job Info
Job Category: Government jobs in Tanzania
Job Type: Full-time
Deadline of this Job: 19 August 2020
Duty Station: Itilima
Posted: 14-08-2020
No of Jobs: 1
Start Publishing: 14-08-2020
Stop Publishing (Put date of 2030): 15-08-2065
Apply Now
Notification Board

Join a Focused Community on job search to uncover both advertised and non-advertised jobs that you may not be aware of. A jobs WhatsApp Group Community can ensure that you know the opportunities happening around you and a jobs Facebook Group Community provides an opportunity to discuss with employers who need to fill urgent position. Click the links to join. You can view previously sent Email Alerts here incase you missed them and Subscribe so that you never miss out.

Caution: Never Pay Money in a Recruitment Process.

Some smart scams can trick you into paying for Psychometric Tests.